Wednesday, October 10, 2018


Andreas Christensen ameonya kwamba huenda akaamua kuondoka Chelsea kama Maurizio Sarri asipompa nafasi ya kucheza.

Andreas Christensen mwenye umri wa miaka 22 msimu uliopita alicheza takribani mechi 40 chini ya Antonio Conte, akijikita kikosi cha kwanza kwenye safu ya ulinzi ya watu watatu.

" Umekuwa msimu mgumu kwangu mpaka sasa. Kiukweli imekuwa ngumu sana. Msimu uliopita ulikuwa mzuri kwangu na nilicheza kombe la Dunia vizuri."

"Siwezi kusubiri zaidi , kuwa na subira. Nina miaka 22 na ni umri ambao nahitaji kucheza. Katika misimu mitatu iliyopita nimecheza sana . Kwahiyo ni wazi kabisa kwamba sioni jinsi gani naweza kubaki kama hali hii itaendelea."

" Ni mapema sana kuongea ni lini nitafanya mabadiliko hayo , lakini ni wazi kwamba sio hali nzuri kwangu ."

0 comments:

Post a Comment