Wednesday, October 10, 2018

Kiungo wa klabu ya Man United, Paul Pogba ameelezea ya moyoni kuhusiana na matazamio ya yeye kuwa kiongozi uwanjani.

Sakata hili limekuja baada ya hivi majuzi kocha mkuu wa Man United Jose Mourinho kutamka wazi wazi kuwa hana mpango wa kumpa Pogba kitambaa cha unahodha tena katika kikosi cha Mashetani wekundu.

Pogba alipohojiwa  hakuweza kuzungumzia kauli hiyo ya Mou bali ameelezea maendeleo yake kwenye timu ya taifa kwani amekuwa akitajwa sana kama kiongozi na mhamasishaji mkubwa sana ndani ya Les Blues. “Sijawahi kuwaza kuwa nahodha timu ya taifa, kuitwa timu ya taifa kwangu ni jambo la heshima zaidi kuliko unahodha"

Pia Pogba ameelezea maoni yake juu ya utofauti wa kiongozi na nahodha "Sio lazima uwe nahodha ili uwaongoze wenzako. kiongozi sio lazima awe nahodha. Sio lazima nahodha awe muongeaji sana uwanjani kwa sababu nimewahi kuona manahodha wengi ambao hawaongei sana," Pogba amejaribu kuweka sawa kuwa kuongea kwake hakumfanyi awe nahodha kwani sio lazima nahodha aongee sana uwanjani. Yeye anaamini anaweza kuwa kiongozi hata kama hana kitambaa cha unahodha.

0 comments:

Post a Comment