Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA) limetangaza kuufungia wimbo mpya wa Mwanza kwa maelezo kuwa unahamasisha masuala yasiyokubalika katika jamii
Katibu Mtendaji BASATA, Godfrey Mngereza amesema leo Novemba 12 kuwa wameufungia wimbo huo na kupiga marufuku kuchezwa mahali popote
Ameongeza kuwa wanawasiliana na mamlaka nyingine ili kuchukua hatua zaidi kwa kuwa tayari wimbo umeenea mitandaoni
Kuhusu kupigwa katika tamasha lao la Wasafi linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 24 mwaka huu amesema nalo watalifungia iwapo watautumia.
0 comments:
Post a Comment