Monday, November 12, 2018

chezaji wa kiungo cha kati wa Ajax Frenkie de Jong, amehusishwa na uhamisho kwenda Manchester City

Manchester City inajitayarisha kumnunua kwa thamani ya £50m katika msimu wa joto mchezaji wa kiungo cha kati wa Ajax mwenye umri wa miaka 21 Frenkie de Jong, licha ya tishio linaloikabili klabu hiyo la uchunguzi kuhusu fedha zake. (Mail)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United Fred, mwenye miaka 25, amemfichulia raia mwenzake wa Brazil mwenye miaka 33 Fernandinho, anayeichezea timu pinzani Manchester City kuhusu changamoto zake katika klabu hiyo. (Metro)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema amemkabili mchezaji wa kiungo cha mbele wa timu hiyo Raheem Sterling baada ya ushindi wa 3-1 katika mechi ya derby dhidi ya Manchester United kwasababu ya kujionyesha au kujigamba kwa mchezaji huyo mwenye miaka 23 katika dakika za mwisho za mechi. (Express)

Everton, Newcastle na West Ham zinataka kumsajili mchezaji raia wa Algeria mwenye umri wa miaka 28 Yacine Brahimi, ambaye kandarasi yake na Porto inamalizika msimu ujao wa joto. (Sun)

Meneja wa Arsenal Unai Emery huenda akampa Eddie Nketiah, 19, nafasi kabla ya kuamua iwapo kuvuka katika dirija la uhamisho Januri ili kumsajili mchezaji wa kiungo cha mbele kuichukua nafasi ya Danny Welbeck aliyejeruhiwa. (Express)

Everton wana wasiwasi kuhusu kujeruhiwa kwa mchezaji wa miaka 29 Gylfi Sigurdsson, aliyeondoka Stamford Bridge akiwa amevaa kiatu cha matibabu baada ya kupigwa chenga na mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea Jorginho katika mechi iliyomalizika kwa sare kati ya pande hizo mbili. (Sun)

Goli la Aleksandar Mitrovic kwa Fulham dhidi ya Liverpool lilikataliwa kihalali lakini goli la Mohamed Salah kwaLiverpool halikupaswa kuidhinishwa utokana na kuwa mpira ulikuwa unasogea wakati kipa Alisson Becker alipopokea free-kiki iliyoishia kuwa goli hilo, kwa mujibu wa aliyekuwa refa katika Premier League Mark Clattenburg. (Mail)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anazungumza na meneja wa England Gareth Southgate kuhusu mlinzi Joe Gomez kukosekana katika mechi ya kirafiki dhidi ya Marekani siku ya Alhamisi wakati mchezaji huyo mwenye miaka 21akiuguzu maumivu kutookana na kuumizwa msuli wa Achilles. (Mirror)

Huenda Manchester City wasipokewe vyema Alhamisi wakati wakurugenzi wakuu wa tim katika ligi kuu England watakapokutana kufuatia tuhuma kuhusu matumizi ya fedha katika klabu hiyo. (Times - subscription required)

Winga wa Bayern Munich Franck Ribery, mwenye umri wa miaka 35, alijibizana na mwandishi wa Ufaransa baada ya timu yake kufungwa 3-2 na Borussia Dortmund Jumamosi. (Bild, via Mirror)

Beki wa kuli wa Paris St-Germain Dani Alves, anasema "haiwezekani" kuwa atakamilisha kazi yake kama mcheza soka ya kulipwa pasi kucheza katika Premier League. (Telegraph)

Ajenti wa kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba anasema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye miaka 25 ameimarisha uhusiano wake na meneja wa klabu Jose Mourinho. (Manchester Evening News, via Raisport)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola aliingilia kati mkataba wa Raheem Sterling kuhakikisha kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 23 anasaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Sunday Mirror)

Chelsea wanataka kumsaini mchezaji mwenye miaka 24 kiungo wa kati wa Barcelona Denis Suarez ambaye meneja wa Blues Maurizio Sarri alijaribu kumsaini wakati wake kama meneja wa Napoli. (Daily Star on Sunday, via Marca)

Arsenal wana mpango wa kumbadilisha kiungo wa kati Aaron Ramsey, 27, na mshambuliaji wa Roma Patrik Schick, 22, mwezi Januari. (Daily Star on Sunday, via Corriere dello Sport)

Meneja wa Bournemouth Eddie Howe ana hofu kuwa beki mwenye miaka 23 Nathan Ake ambaye amehusishwa na Manchester City, Manchester United na Tottenham atauzwa na anatafuta mchezaji wa kuchukua nafasi yake. (Sun on Sunday)

Beki wa Liverpool Andy Robertson atararajiwa kuongeza mshahara wake hadi pauni 60,000 kwa wiki wakati anakaribia kusiani mkataba mpya wa miaka mitano na klabu hiyo. (Sunday Mirror)

Mkataba wa mlinzi wa Manchester United Phil Jones unamalizika msimu ujao lakini klabu lazima ifanye uamuzi kuuongeza kwa mwaka mmoja huku Arsenal and Tottenham wakimmezea mate mchezaji huyo wa maaka 26. (Sun on Sunday)

Barcelona walikataa hata kuzungumzia uwezekani wa Everton kumsajili kiungo wa kati Andre Gomes, 25, kwa mkataba wa kudumu wakati Tottenham walimsaini kwa mkopo msimu wote wakati wa msimu wa joto. (Liverpool Echo)

Wing'a wa England na Borussia Dortmund Jadon Sancho, 18 anasema hawezi kutupa muda kwa mabadiliko ikiwa ataulizwa kuhusu kuhama. (Sunday Express, via Bild)

Mchezaji wa Chelsea Eden Hazard, 27, anasema hana furaha kuhusu kulengwa na wapinzani wakati anaanzz kuhisi madhara ya kucheza mpira. (Sunday Telegraph)

Tamaduni huko Arsenal imebadilika tangu meneja Unai Emery achukue mahala pake Arsene Wenger, kwa mujibu wa kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan, 29. (Sunday Telegraph)

Manchester City inajitayarisha kumnunua kwa thamani ya £50m katika msimu wa joto mchezaji wa kiungo cha kati wa Ajax mwenye umri wa miaka 21 Frenkie de Jong, licha ya tishio linaloikabili klabu hiyo la uchunguzi kuhusu fedha zake. (Mail)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United Fred, mwenye miaka 25, amemfichulia raia mwenzake wa Brazil mwenye miaka 33 Fernandinho, anayeichezea timu pinzani Manchester City kuhusu changamoto zake katika klabu hiyo. (Metro)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema amemkabili mchezaji wa kiungo cha mbele wa timu hiyo Raheem Sterling baada ya ushindi wa 3-1 katika mechi ya derby dhidi ya Manchester United kwasababu ya kujionyesha au kujigamba kwa mchezaji huyo mwenye miaka 23 katika dakika za mwisho za mechi. (Express)

Everton, Newcastle na West Ham zinataka kumsajili mchezaji raia wa Algeria mwenye umri wa miaka 28 Yacine Brahimi, ambaye kandarasi yake na Porto inamalizika msimu ujao wa joto. (Sun)

Meneja wa Arsenal Unai Emery huenda akampa Eddie Nketiah, 19, nafasi kabla ya kuamua iwapo kuvuka katika dirija la uhamisho Januri ili kumsajili mchezaji wa kiungo cha mbele kuichukua nafasi ya Danny Welbeck aliyejeruhiwa. (Express)

Everton wana wasiwasi kuhusu kujeruhiwa kwa mchezaji wa miaka 29 Gylfi Sigurdsson, aliyeondoka Stamford Bridge akiwa amevaa kiatu cha matibabu baada ya kupigwa chenga na mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea Jorginho katika mechi iliyomalizika kwa sare kati ya pande hizo mbili. (Sun)

0 comments:

Post a Comment