Jose Mourinho amekiri kwamba Manchester United wapo kwenye vita ya kuwania nafasi nne za juu msimu huu baada ya kufungwa 3-1 dhidi ya Manchester City.
Baada ya kushinda mechi tatu mfululizo katika mashindano yote jana walifungwa na City dimba la Etihad na sasa wanashika nafasi ya nane katika msimamo , Pointi 7 pungufu ya anayeshika nafasi ya nne na Pointi 12 nyuma ya vinara City baada ya mechi 12.
Alipoulizwa tofauti ya ubora kati ya City na United ni kubwa kiasi gani , Mourinho amesema," Ni pointi 12. Timu yetu inazidi kuboresha kiwango , hata kwa safu ya ulinzi , tunasonga mbele siku hadi siku."
.
. "Tupo nje ya nne bora , tumekabiliana na ratiba ngumu , ugenini kwa Chelsea, ugenini kwa Manchester City , takribani ni ngumu kwa sisi kushinda mechi tatu mfululizo . Sasa inabidi tunyanyuke na kupambana tena ."
Alipoulizwa kama taji ndio limeshatoweka kwao, Mourinho alisema," Tupo nje ya nne bora, tunaanzaje kuongea kuhusu taji ? Kuongea kuhusu taji lazima tuwe ndani ya nne bora, kama siku moja tutaingia nne bora, tutaona tofauti yenyewe."
Alipoulizwa tena kama mbio za ubingwa zimeisha kwake ambapo United wapo karibu zaidi na Cardiff kuliko Man City , Mourinho alitania kwa kusema," Nafikiri hatutoshuka daraja ."
0 comments:
Post a Comment