Arsene Wenger amemkosoa mwamuzi Anthony Taylor kwa kusema amefanya ' uamuzi wa kijinga kwa kuwazawadia Chelsea mkwaju wa Penati kwenye mechi ya sare ya 2-2 jana Usiku.
" Ilikuwa mechi bora sana , kiujumla naamini yoyote angeweza kushinda, majuto ambayo tunayo ni kwamba tulikuwa wa kwanza katika ubao wa magoli ."
" Baada ya hapo tukapata maamuzi ya kijinga na kiakili tukawa tumeshangazwa. Na baada ya hapo tungeweza kupoteza mechi lakini tulikuwa na rasilimali za kurejea mchezoni na mwishoni nadhani ni matokeo sawa kwa kila timu."
" Pindi unapokuja hapa unaona mchezo wa soka , kwa bahati mbaya mechi huwa zinaharibiwa kwa sababu ambazo huwezi kuzielewa."
" Tunachoweza kufanya ni kuendelea kucheza kwa jinsi tunavyotaka kucheza , ni matumaini yangu kwamba kuna hatua itafika maamuzi yatakuwa sahihi na tutapata haki yetu."
Alipoulizwa kama uamuzi wa Taylor ni mbovu zaidi kuliko ule wa Mike Dean ( Penati ) dhidi ya West Brom siku tatu zilizopita, Wenger amejibu . " Uamuzi mbaya au sio mbaya , tunajua tunachopata." " angalia . tangu mwanzo wa msimu . Ndio kitu tunachotakiwa kukubaliana nacho , lazima tukubali na kupigana , lakini hatuwezi kubadilisha ."
" Unaniuliza mimi kama ni Penati . nasema ni uamuzi wa kijinga. unaweza kutoa penati 10 kama hizo katika mechi moja." " Nyie amueni mnavyotaka . Soma magazeti ya nje ya nchi nini watakachoandika , halafu angalia magazeti ya Uingereza, utaona tofauti."
0 comments:
Post a Comment