Mmiliki wa Klabu ya Chelsea FC, Bilionea Roman Abramovich amepewa uraia wa Israeli baada ya Serikali ya Uingereza alikowekeza kusuasua kumpatia Viza
Abramovich ameshindwa kupewa viza kutokana na mzozo wa kidiplomasia kati ya taifa la Uingereza na Urusi, ieleweke kuwa Bilionea huyo alikuwa na uraia wa Urusi
Inaelezwa kuwa imekuwa rahisi kwa mfanyabiashara kupata uraia wa Israeli kutokana na kuwa na asili ya taifa hilo. Amepewa uraia huo kupitia sheria inayowapa kipaumbele watu wenye asili ya Israeli wanaotaka kurejea nchini kwao
Serikali ya Uingereza haitokuwa na kipingamizi kwa mfanyabiashara huyo kwakuwa ataomba viza kama raia wa Uingereza
Roman Abramovich amenunua jumba la kifahari katika mji wa Tel Aviv alikoanzisha makazi yake mapya. (Jamiiforum)
0 comments:
Post a Comment