Friday, June 1, 2018

Royal Family, Prince Harry na Meghan Markle wamekataa zawadi mbalimbali za harusi zenye thamani ya zaidi ya billion 20.7 za Kitanzania na kutaka wahusika warudishiwe zawadi hizo. Taratibu na sheria za royal family ni kuwa zawadi hupokekewa kutoka Tu kwa watu wa karibu na familia lakini waliolikwa kwenye harusi hiyo ambao Sio watu wa karibu na familia hiyo ya kifalme zawadi zao watarudishiwa

Royal family imesema moja ya sababu zawadi kutopokelewa ni baadhi ya makampuni kujipromoti kibiashara kupitia Royal family kitu ambacho hakiruhusiwi. Royal family imesema anayetaka kutoa zawadi aende akatoe msaada kwenye Vituo maalum vyenye watu wanaohitaji msaada ambavyo vimeorodheshwa na familia hiyo ya kifalme

Hata hivyo, siku ya harusi, Royal family badala ya kupokea zawadi toka kwa waalikwa ikawa kinyume Royal family yenyewe ndio ikatoa zawadi ya mifuko/bags kwa wageni  2000  ambapo ndani mlikuwa na zawadi tofauti tofauti Ingawa Sio wageni wote walipewa bags hizo za ni wageni 2000 tu waliopewa zawadi .

0 comments:

Post a Comment