Monday, November 12, 2018

Kwenye wiki ambayo Ousmane Dembele alishindwa kuhudhuria mazoezini na ukosefu wake wa nidhamu , Gerard Pique amesema kwamba ni muda muafaka kumfundisha Dembele kwamba soka ni kazi ya saa 24.

Dembele hakujumuishwa kwenye kikosi cha Barcelona kilichochapwa 4-3 dhidi ya Real Betis jana usiku baada ya kushindwa kuhudhuria mazoezini siku ya Alhamisi , kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania Dembele hakutoa taarifa kwamba alikuwa wapi.

" Hata sisi tulikuwa wadogo sana na tulifanya makosa. Kwa uzoefu wetu lazima tumsaidie kuelewa kwamba mchezo wa soka ni kazi ya saa 24 na lazima aishi kwa mtazamo huo. Ninashawishika kwamba ataboresha kuhusu hilo na uamuzi ambao ameuchukua kocha utamsaidia Dembele kuelewa zaidi."

0 comments:

Post a Comment