Ibrahim Ajibu Migomba (alizaliwa katika mkoa wa Singida tarehe 12 Septemba 1996) ni mchezaji wa klabu ya yanga.
Uwanjani anatumia zaidi mguu wa kulia ingawa anaweza pia kucheza kama winga wa kushoto lakini kiasili Ajibu ni mshambuliaji wa kati.
Ibrahimi ajib alilelewa na mzazi mmoja ambaye ni mama yake pekee,
Baadae walihama Singida kuelekea Dar es Salaam ambako ndiko alikoanzia maisha ya yake ya soka huku akishindwa kupata elimu ya sekondari.
Ulianzia wapi soka?
"Nilianzia soka la ushindani katika ile timu ya Boom FC ya Ilala kwenye Ligi Daraja la Pili na la Kwanza, nikaenda Simba B baadaye nikatimkia Mwadui ya Shinyanga "
"Kisha alirudi tena simba " Alisema ajibu
Ajibu alijiunga kwenye accademy ya klabu ya Simba mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 13 na aliichezea Simba under-20 kabla ya kupandishwa kwenye timu ya wakubwa mwaka 2013 akiwa na miaka 17.
Aliitumikia Simba kwa misimu 4 na kuondoka akaenda kujiunga na club ya Yanga Sc kwa mkataba wa miaka 2 ambao utamweka pale hadi katikati ya mwaka 2019.
Nani ambaye uwezi kumsahau ???
"Namshukuru sana mama yangu, kwani ndiye aliyekuwa akinishikilia sana na kunipa sapoti katika ishu zangu za mpira, yupo Uarabuni lakini amekuwa akiniunga mkono kwa kila nachokifanya."
Ajib kwa sasa ndie mpishi wa magoli ya yanga akiwa pia ndie mchezaji anaongoza kwa ligi yetu kwa pasi za mwisho.
Aliwahi kusifiwa na msemaji wa simba Haji manara kuwa ukiondoa diamond na Ali kiba basi Ajib anashika nafasi ya tatu kwa kutoa burudan
Mtangazi mahiri wa Azam TV Baraka Mpenja alishawahi kumuita Ajib ni mtu alieshushwa na mungu na hakuishia hapo tu akasema ana miguu ya dhahabu .
Nini ndoto zako katika Soka ?
"Ndoto zangu ni kucheza Soka la kulipwa nje ya nchi"
Je unapenda kucheza namba ngapi ?
"Ninaweza kucheza namba zote kiungo mshambuliaji kushoto na kulia ila napenda sana nikipangwa mshambuliaji wa kati no 10"
Taarifa ikufikie Ajib anamkubali sana winga wa kimataifa wa Tanzania saimon msuva ibrahimu ajib ni muumini wa dini ya Kiislamu, ana mke na mtoto 1 wa kike.
Kabla ya hapo alishapoteza mtoto wake mmoja.
0 comments:
Post a Comment