Mbeya derby ni mchezo unao wa kutanisha timu mbili kutoka jiji la mbeya kati ya mbeya city na Tanzania prison.
Watania hawa uwanjani huwa hapatani ilihali wanatumia uwanja mmoja wa sokoine stadium.
Hii inatokana na changinzo kubwa la mashabiki majukuani. Mbeya city timu ya kizazi kipya waitavyo mashabiki wake na Tanzania prizon timu ya magereza mashabiki wao huwa hawapikiki chungu kimoja.
SABABU ZA UTEMI NINI?
Sababu kubwa hasa ni aina ya mashabiki wa pande zote mbili .
Mashabikibwa mbeya city ni vijana tena wengi ni wahuni wa standa na mitaani walio jawa na morali ya ushangilia na fujo nyingi za hapa na pale nje na ndani ya uwanja.
Mbeya city inasadikika kushangiliwa sana na watu wa uswazi tena wengi maskini au kipato kidogo na wengi wao hawana kazi.
Kwa upande wa mashabiki wa Tanzania prison wai ni wamejaa maafande wa magereza , wanajeshi na polisi.
Inasemekama pia watu wenye uwezo na wenye kazi nzuri wastaarabu na wazee huishabikia sana Tanzania prison.
UHASAMA WAO UMEANZIA WAPI?
Kama ujuavyo wahuni na polisi hawa endani kabisa basi uko ndo chanzo cha ugomvi.
Mashabiki wa mbeya city hushangilia kwa nguvu na morali ya juu na hivyo hivyo kwa mshabiki wa prison. Morali inapo panda hujikuta na visilani vya ugomvi huamka.
Lakini pia maskini hutaka kumfunga tajili hivyo mbeya city hupigana iifunge Prison wakongwe lakini nao prison hawataki kuabishwa na watoto.
Hivyo basi hupelekea mechi kuwa ya nguvu kiushindani na hutawaliwa na akili nyingi na undava undava mwingi kwa mabeki na viungo wakabaji.
REKODI ZAO ZIKOJE?
Mbeya city na Tanzania prison wamekutana mara tano huku prison akishinda michezo 2 na kwenda sare mara tatu. Mbeya city hajawahi ibuka na ushindi dhidi ya Tanzania prison.
0 comments:
Post a Comment