Thursday, July 26, 2018

Klabu ya singida united yatolea ufafanuzi wa mchezaji Elisha moroiwa. Kupitia ukurasa wao instagram

"Mchezaji wetu huyu kwa makubaliano ya awali ya viongozi wa Yanga na Singida United alitakiwa ajiunge na Yanga kwa msimu ujao, makubaliano haya yalilenga kuimarisha safu ya ulinzi ya Yanga hususani kwa kipindi hiki cha kombe la shirikisho na ligi msimu ujao baada ya viongozi wao kusema kunaupungufu wa beki kwenye kikosi hicho."

"Kama klabu tulifanya taratibu zote za kumpeleka mchezaji huyo Yanga kama makubaliano yalivyokuwa."

"Dakika za mwisho kuelekea kufungwa kwa usajili,Elisha Muroiwa  beki huyu wa timu ya Taifa ya Zimbabwe aliyeiongoza Zimbabwe kwenye michuano mikubwa ya AFCON 2017 kule Gabon AMEKATALIWA na Viongozi wa YANGA kwa madai kwamba kwa sasa wanabeki wa kutosha hivyo hawahitaji tena huduma ya beki huyu."

"Muroiwa atabaki kuwa mchezaji wa Singida United kwa misimu miwili ijayo." imetolewa na afisa habari wa  singida united

0 comments:

Post a Comment