Tuesday, March 5, 2019



Simba wako tayari kwa ajili ya mechi yao dhidi ya JS Saoura ya Algeria na kinachofuatia ni safari.


Maana tayari wamemaliza maandalizi na kinachofuata ni kumalizia mambo kadhaa watakapokuwa nchini Algeria.


Leo mapema wamefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Boko Veterani, mchana wa leo kitaanza safari yake ya kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Soura.


Simba inaenda kucheza mechi hiyo ya marudiano ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 3-0 walioupata katika mchezo wao wa kwanza kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.



Kwa mjibu wa Kocha wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems amesema kuwa msafara wake utakuwa na wachezaji wasiopungua 20 na benchi lake la ufundi.

0 comments:

Post a Comment