Saturday, December 23, 2017

Barcelona wameizidi Real Madrid pointi 14 kileleni mwa msimamo wa La Liga baada ya kushinda 3-0 Clasico ya Jumamosi kwenye uwanja wa Bernabeu

Luis Suarez alianza kufungua ukurasa wa mabao akimalizia pasi ya Sergi Roberto muda mfupi tu baada ya mapumziko,

Lionel Messi akiipatia Barcelona goli la pili kwa mkwaju ya penalti baada ya Dani Carvajal kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuushika mpira uliopigwa na Paulinho.

Real Madrid hawakuweza kujibu mapigo baada ya kupunguzwa watu 10, na Barcelona walimuingiza Aleix Vidal ambaye aliipatia timu bao la tatu baada ya Keylor Navas kushindwa kuujaza mikononi mpira dakika za majeruhi.

0 comments:

Post a Comment