Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema anaamini kuwa kikosi chake hakitamaliza Ligi bila kushindwa baada ya ushindi wao wa 18 mfululizo kufika kikomo walipotoka sare ya sufuri na Crystal Palace
City waliadhibiwa kwa penalti dakika za mwisho lakini kipa Ederson aliuokoa mkwaju wake Luka Milivojevic.
Sare hiyo inadumisha rekodi yao ya kutoshindwa msimu huu kuwafungua mwanya wa pointi 14 kileleni.
Arsenal ilimaliza ligi ya mwaka 2003-2004 bila kushindwa lakini Gurdiola anaamini kuwa Manchester City haiwezi kufikia hilo.
"Sifikiri kuwa sitashindwa," alisema Guardiola. "Hilo haliwezi kufanyika.
Labda Wenger ana hofu kuhusu hilo lakini ninamuambia mara nyingi kuwa rekodi ya mwaka 2004 ni yake.
"Kuna timu ngumu zaidi, ushindani mkali na mechi nyingi."
0 comments:
Post a Comment