Wednesday, July 18, 2018

Alex Oxlade-Chamberlain atakosa sehemu kubwa  ya msimu ujao wa 2018/2019 akiwa anaendelea kuuguza jeraha lake, Liverpool wametangaza.

" Sasa hivi tunaona ni muda sahihi kuwaambia watu kwamba kwa Ox msimu huu unaoanza kwake itakuwa kuhusu kupona jeraha lake kwanza " Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema hivyo kupitia tovuti ya Liverpool.

" Tulijua hili tangu siku ambayo aliumia na baada ya upasuaji wa mafanikio , tulikuwa tuna uhakika. Ni matumaini yetu kwamba kila mmoja wetu achukilie taarifa hii kwa uwajibikaji na utulivu."

0 comments:

Post a Comment