Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Ibrahim Ajib ni mchezaji anayetumia akili nyingi anapokuwa dimbani.
Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Alliance, Zahera amesema Ajib ana uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi anapokuwa na mpira na hadhani kama kuna mchezaji anayeweza kumfikia hapa Tanzania. "Kwa wachezaji wote wanacheza ligi kuu Tanzania hapa hakuna ata mmoja anaweza kuwa na akili ya mpira kama aliokuwa nayo Ajibu," amesema Zahera "Yeye kabla hujampatia mpira tayari ameshajua nini aufanyie, kinachotakiwa sasa na aongeze nguvu sana na kupambana vyakutosha ili awe bora zaidi." Ajib amehusika katika mabao yote matatu ya Yanga kwenye mchezo dhidi ya Alliance, akifunga moja na kutengeneza mawili.
Hata hivyo Zahera amemtaka Ajib kuwa na mwendelezo wa kiwango wa chake. "Ajib anahitaji kubadilika. Awe na mwendelezo wa kiwango chake. Sio leo anafanya vizuri kesho anashuka chini. Inatakiwa awe anapanda kila mchezo"
Alipoulizwa kuhusu maoni yake kama anaona ni wakati sahihi kwa Ajib kuitwa timu ya Taifa, Zahera amesema hana shaka kuwa Ajib anaweza kuchezea timu ya Taifa.
Lakini amemtaka aongeze juhudi na kujituma zaidi anapokuwa dimbani kwani kucheza timu ya Taifa si 'lelemama'
0 comments:
Post a Comment