Aliyekuwa mchezaji mkongwe zaidi kwenye kikosi cha Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' ameteuliwa kuwa Meneja wa mabingwa hao wa kihistoria Tanzania Bara.
Hafidh Saleh aliyekuwa anakishikilia cheo hicho amebadilishiwa majukumu na sasa ni Mratibu.
Nadir ameitumikia Yanga kwa miaka 12, ndiye mchezaji anayeshikilia rekodi ya kucheza Jangwani kwa muda mrefu zaidi akifuatiwa na Fred Mbuna aliyedumu Yanga kwa miaka 11.
Nadir amekuwa nahodha wa kikosi cha Yanga kwa zaidi ya miaka minne. Sasa ataendea na majukumu yake lakini akiwa kiongozi nje ya uwanja.
0 comments:
Post a Comment