Manchester United na Valencia wote wataimgia katika mchezo wa Jumanne wa UEFA Champions League wakiwa na uhitaji mkubwa wa matokeo chanya baada ya wote kuanza msimu vibaya.
Red Devils hawajashinda mechi hata moja katika mechi 3 zilizopita kwenye mashindano yote, kikiwemo kipigo cha 3-1 vs West Ham.
Los Che kwa upande wao hatimaye walimaliza ukame wa kutoshinda katika 4 zilizopita kwa kushinda vs Real Sociedad lakini hawakucheza vizuri kabisa Katika mchezo huo walioshinda 1-0.
Valencia ambao walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kuwapa upinzani mkubwa United na Juventus wakati kundi lao lilipotangazwa. Lakini hali imekuwa tofauti kwa kuanza msimu isivyotarajiwa.
Valencia walitegemewa kuwa wakali sana kwenye mchezo wa kushambulia hasa baada ya usajili wao kufanikisha washambuliaji Guedes na Rodrigo wamebakia kwenye klabuni.
United wao wameanza ligi vibaya kuliko wakati mwingine wowote tangu Premier League ilipoanza.
Wanashika nafasi ya 10 baada ya mechi 6 za ligi, tayari wameachwa pointi 9 na viongozi wa ligi - Manchester City na Liverpool. Kipigo chao dhidi ya Hammers kimezidi kuongeza joto la kutaka Mourinho afukuzwe.
0 comments:
Post a Comment