Wednesday, July 18, 2018

Klabu ya Liverpool imekubaliana na klabu ya Roma kumnunua kipa Alisson(25) kwa ada ya takribani Paundi Milioni 66.8

Liverpool sasa wanatarajiwa kuanza kufanya mazungumzo kwa ajili ya makubaliano binafsi na kipa huyo raia wa Brazil

Dau la Liverpool kwa kipa huyo ambalo ni takribani Euro Milioni 70 litavunja rekodi inayoshikiliwa na dau la Juventus kwenda Parma la mwaka 2001(Euro Milioni 53) kwa ajili ya kumnunua Gianluigi Buffon

Aidha kwa ligi ya England dau la kipa linaloshikilia rekodi ni dau la Euro Milioni 40 lililolipwa na Manchester City kwenda Benifica kwa ajili ya kipa Ederson

0 comments:

Post a Comment