Saturday, July 28, 2018

Baada ya mwanamitindo Jokate Mwegelo pamoja na aliyekuwa msemaji wa Yanga Jerry Murro kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa Wakuu wa Wilaya, mashabiki na wadau katika mitandao ya kijamii wanambeza Steve Nyerere kwa kuwa amekosa kuteuliwa.

Muigizaji huyo amekuwa akionekana katika matukio mengi akitetea utendaji wa Rais Magufuli hali ambayo iliwajenga picha mashabiki hao kwamba anataka nafasi ya uongozi.

Steve baada ya kupokea meseji nyingi za kubezwa, amedai yeye hamsupport Rais Magufuli ili apewe nafasi ya uongozi anafanya hivyo kwaajili ya kusaidia na kuunga mkono harakati zeke.

“Mnao nitumia meseji za pole naomba iwe mwisho sasa. Sipo kwa ajili ya cheo nipo kwa ajili ya Watanzania kwanza mengine no, msinilishe maneno,” aliandika Steve Nyerere kupitia Instagram yake.

Muigizaji huyo alikuwa mmoja kati ya wasanii ambao walimpigania Rais Magufuli katika uchaguzi mkuu uliopita.

0 comments:

Post a Comment