Manchester United huenda wakahamia kwa beki wa kimataifa wa Colombia Yerri Mina kama wakishindwa kupata saini ya Harry Maguire au Toby Alderweireld, kwa mujibu wa taarifa kutoka Daily Mirror.
Kama Maguire , Mina nae alikuwa na fainali nzuri za kombe la Dunia akifunga mara tatu pamoja na lile goli la dakika za majeruhi dhidi ya Uingereza.
Mina anatarajiwa kuondoka Barcelona wiki ijayo licha ya kuhamia Nou Camp mwezi Januari mwaka huu.
Everton na Lyon wamehusishwa na kutaka saini ya beki huyo wa kati lakini United huenda akawapiku wote wawili majira haya ya kiangazi.
0 comments:
Post a Comment