Wednesday, September 26, 2018

Mimi ni mtoto wa Mwanadiplomasia ambaye nilizaliwa nchini Senegal. Wazazi wangu walihamia Ufaransa mimi nikiwa na umri wa mwaka mmoja.

Nilipokuwa mdogo wakati naanza maisha yangu ya mpira wa miguu nilienda kufanya majaribio kwenye timu ya Paris St. Germany (PSG). Nilifanikiwa kufanya majaribio ila miongoni mwa Makocha wa timu hiyo ya PSG aliniambia

"Wewe ni kijana mzuri  lakini una umbo dogo ambalo huwezi kucheza mpira".

Niliumia sana alivyoniambia vile nikarudi nyumbani bila furaha.

Baada ya kujitafakari niliamua kuruka kama Kangaroo kutoka katika hali ya kuamini alichoniambia yule Kocha na kuamini kwamba naweza kucheza na kufika mbali. Ninachotakiwa ni kutokukata tamaa. Nacho mshukuru Mungu alinipa uwezo wa kubadilisha mawazo hasi kuwa chanya.

Mpaka leo nimefanikiwa kuvichezea vilabu vikubwa duniani, vikiwemo Monaco, Nice, Manchester United, Juventus, Marseilles na West Ham United.

Naweza kusema ni mafanikio makubwa sana kwangu. Laiti ningebaki na mawazo ya yule Kocha aliyeniambia kwamba siwezi mpira pengine leo nisingekuwa hapa. Katika maisha yangu nimejifunza fika kuwa kama mtu anasema huwezi kufanya kitu haitakiwi kukurudisha nyuma bali ni kujiamini na kutenda.

Nisingefanikiwa kuweka historia kwenye vilabu nilivyochezea na timu yangu ya Taifa ya Ufaransa kama ningebaki na yale mawazo kwamba siwezi kucheza mpira. Na ufupi pamoja na udogo wangu nimeweza kucheza sehemu kubwa kubwa na kuweka historia katika timu hizo. - Patrice Evra

0 comments:

Post a Comment