Yanga imeendelea kujifua mkoani Morogoro huku kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera akitilia mkazo mazoezi ya kuongeza pumzi.
Asubuhi leo Jumatano, Yanga wamefanya mazoezi katika Uwanja wa Jamhuri, ambapo kocha Zahera ameonekana akianza na mazoezi ya kuongeza pumzi.
Katika mazoezi hayo Zahera ameonekana akiwanya wachezaji wake katika makundi mawili moja likisimamiwa na mwenyewe huku lingine likisimamiwa na msaidizi wake, Noel Mwandila.
Kocha Zahera ameonekana kutaka kuona mchezaji anakimbia kwa kufuata muda aliotaka yakiwa ni mazoezi ya mbio za kasi.
Kila mchezaji alihudhuria mazoezi hayo isipokuwa makipa pekee ambao walikuwa na mazoezi yao na kocha wao Juma Pondamali.
Mpaka sasa Yanga inaonekana haina mchezaji majeruhi ukiondoa Juma Abdul na Juma Mahadhi ambao bado hawajajiunga na timu hiyo. (Mwanasport)
0 comments:
Post a Comment