Nyota wa Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania Isco ameruhusiwa toka hospitali hivi leo baada ya kufanyiwa upasuaji. .
Isco alikumbwa na maumivu makali ya tumbo siku ya jumanne ambapo baada ya kukutana na wataalam wa afya aligundulika kuwa na tatizo la kidole tumbo "acute appendicitis".
Baada ya kufanyiwa upasuaji huo klabu imeeleza kuwa Isco atakosa mchezo dhidi ya Sevilla, huku muda atakaokaa nje ya dimba bado haujawekwa wazi lakini inadhaniwa ikawa mwezi mmoja , Michezo mingine inayotajwa Isco ataikosa ni ile ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya CSKA Moscow na Viktoria Plzen.
Akizungumza na vyombo vya habari Jana Jumanne Kocha wa klabu hiyo Julen Lopetegui ameonyesha matumaini makubwa kuwa Isco hatakuwa nje kwa muda mrefu. Aidha anaimani kubwa na wachezaji wengine waliobaki.
" Tunakikosi kizuri mtu mwingine atacheza .ninaujasili na wachezaji wangu waliobaki "
0 comments:
Post a Comment