Thursday, October 11, 2018

Kocha Leonardo Jardim ametimuliwa kazi na klabu ya AS Monaco baada ya kuiongoza klabu hiyo kupata ushindi katika mchezo mmoja pekee msimu huu.

Jardim alijiunga na Monaco mwaka 2014 na kuiongoza Monaco kufika hatua ya Nusu fainali kwenye michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2016-17.

Pia kocha huyo aliisaidia klabu hiyo kuchukua ubingwa wa France league 1 msimu uliopita ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu walivyofanya hivyo mara ya mwisho  mwaka 2000.

Klabu ya Monaco imemfukuza kazi kocha Leonardo Jardim baada ya kuwa na mwanzo mbaya katikusimu.

Nyota wa zamani wa Arsenal na Barcelona Thierry Henry ndio anapewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba yake.

0 comments:

Post a Comment