Kiungo wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan atakosa mechi ya Europa League alhamisi hii mjini Baku kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya Armenia na Azerbaijan wakigombania jimbo la Nagorno-Karabakh.
Kutokana na mgogoro huo raia wa Armenia hawaruhusiwi kuingia nchini Azerbaijan.
Kwa sababu hizo za kiusalama kiungo huyo wa Armenia imemlazimu kutosafiri kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Qarabag FK.
Licha kukosekana kwa Mkhitaryan ,Arsenal bado wana kikosi kizuri kushinda mchezo huo,lakini kocha Unai Emery inabidi afahamu
kuwa fainali ya michuano hiyo ya Europa League msimu huu itapigwa kwenye uwanja huo huo watakaocheza Alhamisi
Mgogoro huu baina ya Armenia na Azerbaijan awali ulianza mwanzoni mwa karne ya 20.
Na huu unaoendelea sasa umeanza mwaka 1988 ambapo 'Karabakh Armenians' walidai Karabakh imetolewa kutoka Soviet Azerbaijan na kwenda Soviet Armenia.
Mgogoro huo ulizidi kuwa mkubwa zaidi miaka ya awali ya 1990
0 comments:
Post a Comment