Manchester City wameupa jina mmoja wa uwanja katika viwanja vyao vya mazoezi , JOE HART kwa kutambua mchango wa Golikipa wao wa zamani.
Picha iliyotumika kuwekwa katika uwanja huo ni ile ambayo Hart alikuwa akishangalia walipofunga goli ambalo lilisaidia kutwaa taji la EPL 2012 baada ya miaka 44.
Hart pia atakabidhiwa kadi ya msimu mzima ya maisha yake yote ya kumuwezesha kuingia uwanjani hapo bure pindi Man City watakapomenyana dhidi ya Burnley kesho.
Hart aliitumikia Man City kwa kipindi cha miaka 12 na kutwaa mataji mawili ya EPL,kombe moja la FA na mawili ya Carabao.
Joe Hart aliondoka Etihad kufuatia kuto elewana vizuri na pep guardiola na kumwachia nafasi Bravo nakutolewa kwa mkopo huko seria A. Hata hivyo bravo aligeuka shati kufutia kufungwa magoli mengi ya mbali na kupelekea nafasi hiyo kuchukuliwa na Erdison mpaka sasa.
0 comments:
Post a Comment