Mkuu wa Mkoa wa Mtwara GELASIUS BYAKANWA, ameamua kuuweka pembeni kimajuku uongozi wa timu ya soka ya NDANDA FC ya mkoani Mtwara kutokana na kutokua na uwezo wa kuihudumia timu hiyo.
Akitangaza maamuzi hayo leo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema maamuzi hayo hayajaingilia katiba ya klabu hiyo, na kwamba majukumu ya kuiendesha timu hiyo yamekabidhiwa kwa kamati ya watu 10 aliyoiunda inayoongozwa na Mwenyekiti LAURENT WEREMA.
Mkuu huyo wa mkoa amemwomba msanii Harmonize ajiunge kwenye kamati hiyo ya uendeshaji wa timu ya ndanda fc.
0 comments:
Post a Comment