Pep Guardiola amemuomba msamaha Gabriel Jesus kwa kumzuia kupiga penati ambayo Riyad Mahrez alikosa kwenye mechi ya sare ya 0-0 dhidi ya Liverpool.
Huku mpigaji penati maalumu wa Man City , Sergio Aguero akiwa kwenye benchi badaa ya nafasi yake kuchukuliwa na Jesus kipindi cha pili , Jesus alionesha nia ya kutaka kupiga penati ambayo kama angefuka ingewapa Man City ushindi wao wa kwanza ndani ya Anfield tangu mwaka 2003.
Hata hivyo Guardiola aliamua vingine kupitia Benjamin Mendy kwamba Mahrez ndio apige penati . Usajili huo wa Pauni Milioni 60 alipaisha penati hiyo, ikiwa penati yake ya tano kukosa katika nane za mwisho alizopiga.
Baada ya mechi Guardiola alisema," Kila tukifanya mazoezi kila siku Mahrez amekuwa akipiga penati vizuri na kufunga na hiyo ilinipa imani kubwa kwamba atafunga . Itakuwa uzoefu mzuri kwake kukosa. Siku nyingine atafunga."
"Jesus alitaka kupiga penati . Namuomba msamaha . Ulikuwa uamuzi wangu."
0 comments:
Post a Comment