Nahodha wa Yanga Kelvin Yondani jana alikosa mazoezi ya kikosi hicho kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Simba baada ya kuugua ghafla.
Hali hiyo iliizua hofu miongoni mwa mashabiki wa mabingwa hao wa kihistoria wa soka Tanzania kutokana na umuhimu wake kwenye mchezo huo.
Habari njema ni kwamba madakatari wa Yanga wamehakikisha Yondani hakosekani kwenye mchezo wa keshokutwa baada ya kumfanyia tiba ya maradhi ya malaria yaliyokuwa yanamnyemelea.
Meneja wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema Yondani yuko sawa kiafya na leo amefanya mazoezi na wachezaji wengine kama kawaida.
0 comments:
Post a Comment