Friday, October 19, 2018

Real Madrid tayari imefanya Mazungumzo na aliyewahi kuwa kocha mkuu wa Chelsea, Antonio Conte juu ya kuja  kuwa mbadala ya kocha wa sasa wa klabu hiyo Julen Lopetegui, ambaye kapewa mechi tatu tu kuokoa  kibarua chake..Kwa mujibu wa Corriere dello Sport huko nchini  Italia.

Lopetegui kapewa mechi tatu kuokoa Kibarua chake ambazo ni , October 20 - Real Madrid vs Levante (Laliga), October 23 - Real Madrid vs Viktoria Plzen (UEFA), na October 28 - Barcelona vs Real Madrid (Laliga).

Mabosi wa Real Madrid wameamua kufanya baada ya kutofurahishwa na Matokeo ya Klabu yao chini ya kocha huyo.

Madrid wamepoteza mechi tatu katika mechi nne zilizopita, wamepigwa na Sevilla, CSKA Moscow na Alaves, huku Katika Msimamo wa Laliga wapo Nafasi ya Nne Katika mechi Nane walizocheza.

Real Madrid walimtangaza Lopetegui kuwa kocha wao mpya Kipindi anainoa timu ya Taifa ya Hispania, Kipindi hicho zilibakia Siku chache kuanza Kwa Kombe la Dunia, Kwa kitendo Shirikisho la soka Hispania likatangaza kumfuta kazi kocha huyo baada ya kusaini Madrid bila ruhusa ya Waajili wake, Alifukuzwa zikiwa zimesalia Siku Takribani Mbili kuanza Kwa Kombe la Dunia.

Na Sasa Lopetegui ana mechi tatu kuokoa Kibarua chake kuepuka kutimuliwa Mara ya pili Katika mwaka Mmoja, lazima ashinde mechi Dhidi ya Levante, kisha ashinde vs Viktoria Plzen katika UEFA, na mechi ya mwisho kuwafunga Barcelona kwenye mechi ya El Clasico.

Antonio Conte 49, kwasasa hana timu baada ya kuachwa na Chelsea Ambayo kaifunza Kwa miaka Miwili, na sasa anatajwa kuwa ndiye chaguo la kwanza Kwa mabosi wa Real Madrid kwenda kuinoa Klabu yao. @lugoha sport

0 comments:

Post a Comment