Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesogeza mbele tarehe ya mwisho ya zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kugombea Uongozi katika Klabu ya Young Africans.
Zoezi hilo limeongezwa siku 5 na sasa litakwenda mpaka Novemba 19,2018 ambapo awali zoezi lilikuwa linafikia tamati leo Novemba 14,2018.
Wanachama tayari wameanza kujitokeza katika zoezi hilo la uchukuaji na urudishaji wa fomu.
Aidha Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Young Africans zinatarajia kukutana Ijumaa Novemba 16,2018
Uchaguzi wa Young Africans unatarajia kufanyika Januari 13,2019 nafasi zinazogombewa zikiwa ni Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti na Wajumbe 4 wa Kamati ya Utendaji.
0 comments:
Post a Comment