Tuesday, January 15, 2019

TFF yajadiliana na Wanachama waliofungua kesi Mahakamani

Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Malangwe Mchungahela amesema Kamati yake inajadiliana na Wanachama wa Yanga waliofungua kesi Mahakamani kupinga uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi zilizowazi katika klabu ya Yanga.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mchungahela amesema Wanachama hao wameridhia kufuta kesi walizofungua Mahakamani huku makubaliano yakifikiwa kufanyia kazi hoja ya kadi za Wanachama zinazopaswa kutumika kwenye uchaguzi huo.

Mchungahela amesema mchakato wa uchaguzi wa Yanga utaendelea kama kawaida baada ya siku saba kuanzia jana

Katika hatua nyingine Mchungahela amesema miongoni mwa Wanachama watatu waliofungua kesi Mahakamani, wawili sio wanachama halali wa klabu ya Yanga.

0 comments:

Post a Comment