Monday, March 18, 2019

Klabu ya Yanga imepanga kukusanya shilingi bilioni 1.5 kutoka kwa wanachama na mashabiki wake nchi nzima ikiwa ni awamu ya pili ya kampeni ya uchangiaji kwaajili ya kuiendesha timu hiyo.

Mkakati huo umewekwa bayana leo katika kikao cha kwanza cha kamati ya uzinduzi na uhamasishaji rasmi wa kampeni ya kuichangia timu hiyo awamu ya pili chini ya mwenyekiti wake Anthony Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini.

“Pamoja na mipango na mikakati mipya mizuri iliyowekwa kwenye kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati Mh. Antony Mavunde aliainisha mpango mpya wa kukusanya kiasi cha Tsh 1.5B kutoka kwa wanachama na mashabiki wa Yanga mikoa yote nchini”, imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa leo na klabu hiyo. ( Source Yanga IG and Azam Tv )

0 comments:

Post a Comment