Gyan ni mchezaji Raia wa Ghana aliyetua simba msimu uliopita kuja kuongeza nguvu enzi za kocha Omog. Gyan alitua Simba sc kucheza nafasi ya ushambuliaji.
Uongozi ulipo badilika alibadilishiwa majukumu na kuwa kiungo mkabaji. Amehudumu hapo mpaka simba ikatwaa kikombe cha ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita.
Mwanzoni mwa Msimu huu akasajiliwa kocha mwingine ambaye ni Patrick Aussems ameonekana kutovutiwa na kiwango cha Gyan sana licha ya kupiga kazi nzito eneo la kiungo na kumpelekea kumbadalishia majukumu na kumchezesha kama beki wa pembeni.
Kwa michezo kadhaa aliyochezeshwa nafasi ya ulinzi wa pembeni ameonekana kuimudu vizuri kabisa ikiwemochezo wa leo dhidi ya Mtibwa sugar.
Gyan ameonesha halii ya utii katika kwa makocha wote wa tatu lakini bado hazungumzwi sana midomoni mwa mashabiki kama ilivyo kwa wachezaji wengine.
Tetesi kutoka ndani ya klabu zinadai eti ni moja kati ya wachezaji watakao pewa mkono wa kwa heri mwishoni mwa msimu huu.
Wachezaji wengine wanao husuishwa na kuondoka simba ni pamoja na :-
1. Bocco
2. Mlipili
3. Kwasi
4. Kaheza
5. Bukaba
6. Zana coulibaly
0 comments:
Post a Comment