Wednesday, May 8, 2019

Katika mchezo wa leo Tumeshuhudia wachezaji wawili wa simba sc Okwi na Kagere wakifunga hat-trick kila mmoja. Okwi ndiye alikuwa wa kwanza kupiga hat-trick.

Mpira ulipo isha wote wakapewa mpira mmoja mmoja. Ina maana mipira imetoka miwili.

Kisheria mwamuzi hakuwa sahihi kabisa. Ikitokea wachezaji wawili wamepiga hat-trick katika mchezo mmoja iwe wite wa timu mmoja au  mmoja kutoka timu pinzani basi anaangaliwa yule aliye funga hat-trick mapema zaidi.

Kwa nini, sababu mpira unao takiwa utolewe ni ule mmoja uliopo mchezoni pindi mpira unapo malizika.

Hivyo basi, katika mchezo wa leo aliye stahili kupewa mpira ni  Emanuel okwi tu kwa sababu alikamilisha Golo lake la tatu (  hat-trick) dakika ya 47 huku kagere akikamilisha hat-trick ya 83.

0 comments:

Post a Comment