WanaYanga mnaelekea kupata mafanikio mnaanzisha chochoko zisizo na maana. Kuhusiana na Msemaji wa timu mzigo mnao mtwisha siyo wake ni wa kwenu.
Jukumu la kwenda uwanjani ni la mashabiki tena bila kulazimishwa. Mapenzi ya shabiki huonekana anapo ishangilia timu yake basi.
Wanayanga wengi kwa miaka miwili hamuonekani uwanjani eti tu msemaji wa timu haja kuambia uende. Swali ni je huyo msemji alikulazimisha kuishabikia Yanga ? Jibu ni hapana.
Utamaduni wa Simba sc na Yanga sc mashabiki hujaa uwanjani pale tuu timu inapofanya vizuri ikiyumba tu na wao wanayumba.
Kipindi simba sc inafanya vibaya mashabiki hawakuonekana kwa wingi kuja kuipa nguvu timu yao swali ni je Huyo msemaji wao hakuwepo ?. Kuna uroho wa madaraka unajionesha tena waziwazi wanayanga waepukeni hawa watu wataleta migogoro isiyo na tija klabuni.
Sunday, August 11, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment