kikosi cha yanga kimerejea salama dar es salaam kikitokea mkoani mtwara mara baada ya kumalizana na ndanda fc kwa mchezo wa ligi kuu ulioisha kwa yanga kuibuka na ushindi wa goli 1 - 0.
Ikiwa kigi ipo mapumzikoni kupisha michuano ya kimataifa , kaimu kocha mkuu wa yanga charles Mkwasa aliomba vijana wake wapate angalu mchezo mmoja wa kujipima nguvu kabla ya kuvaana na Jkt Tanzania siku ya jumatano.
Afisa habali wa yanga Hassan Bumbuli ameweka wazi kuwa yanga itacheza na coastal union ya tanga siku ya jumapili uwanja wa uhuru.
Aidha mkwasa atautumia mchezo huo kuwajaribu baadhi ya wachezaji ambao hakuwa nao mtwara kwa matatizo mbalimbali na kurekembisha makosa kuelekea mchezo wa ligi kuu jumatano
0 comments:
Post a Comment