TATHIMINI: FALCAO NI MTU HATARI, MIGUU YAKE ITATOA MABAO 15+
Foot-work yake ipo safi , ana uwezo wa kumiliki mpira vizuri ana-struggle sana uwanjani hakai sehemu moja ya uwanja licha ya kuwa ni namba 9 lakini anacheza kisasa zaidi.
Siku ya jana nilitenga mda wa kumwangalia nikiwa na jamaa zangu kiukweli wengi dakika za mwanzoni walimwona hana lolote licha ya kuto poteza pasi hata moja.
Kadri mda unavyoenda alionekana kuongezeka kasi na ana touch nzuri sana ya mpira bahati mbaya tu aliangushwa sana wings za jana hakutendewa haki kabisa, hakulishwa ipasavyo.
Kaseke alionekana kukimbia kwa kasi sana ila akifika langoni mwa adui hamwagi maji ( cross) vizuri7 marakadhaa alipiga cross zilizo ishia miguuni mwa walinzi.
Safari ya falcao na ifananisha na ile ya Chirwa. Chirwa alitua jangwani kwa dau kubwa sana ila michezi ya mwanzoni alikosa fitness kabisa kiasi cha mzee AkilImali shabiki wa Yanga lialia kusema wamepigwa kadri mda ulivyo enda alionekana hatari zaidi na kuwa kipenzi cha mashabiki.
Utabiri wangu miguu ya Falcao itazaa mabao zaidi ya 15+ msimu ujao. Kulingana na aina ya wachezaji watakao msaidia ndani ya kikosi cha Yanga sc.
0 comments:
Post a Comment