Jurgen Klopp amewasisitiza nyota wake kuwa makini kwenye ulinzi wakati watakapovaana na Arsenal kwenye uwanja wa Emirates.
Mara ya mwisho Majogoo kwenda London Kaskazini walipokea kipigo cha magoli 4 kwa 0 dhidi ya Spurs mwezi wa kumi lakini baada ya hapo Liverpool imeruhusu goli 4 pekee katia mechi 8 kwenye Ligi kuu.
Itakuwa ni kama mechi ya kisasi kwa Arsenal kwani mechi ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa mwezi Agosti na Washika bunduki hao walipokea kipigo cha magoli 4 kwa 0, magoli kutoka kwa Roberto Firmino, Sadio Mane, Mohamed Salah na Daniel Sturridge.
0 comments:
Post a Comment