Harry Maguire alifunga goli la kusawazisha dakika ya 94 Manchester United walipadhibiwa kwa kupoteza nafasi kwenye sare ya 2-2 dhidi ya Leicester
Jamie Vardy alifunga goli safi kwa shambulizi la kushtukiza dakika ya 27 - Goli lake la 50 kwenye Ligi Kuu Uingereza, na la nne katika michuano yote dhidi ya United.
United walijibu dakika 13 baadaye baada ya Juan Mata kuweka kimiani baada ya kazi nzuri kutoka kwa Jesse Lingard, kablaya Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Hispania kupiga mpira wa adhabu ulizama moja kwa moja baada ya saa moja kuiwezesha United kuongoza.
Leicester walishinikiza kupata goli la kusawazisha, lakini Daniel Amartey aliyetokea benchi alipata kadi nyekundu isiyokuwa na sababu baada ya kuingia mara mbili kwenye kitabu cha mwamuzi, ilione kama United wangepata magoli zaidi.
Lakini vijana wa Jose Mourinho
walipoteza nafasi nyingi kupata, Maguire alimaliza mchezo kwa kugawana pointi baada ya kufanya kazi njema kusawazisha dakika ya 94.
Kwa matokeo hayo, United sasa wanakuwa nyuma ya Manchester City kwa pointi 13, Leicester wakibaki nafasi ya nane.
Lukaku alikuwa kiunganishi safi cha United kufanya vizuri kwenye uwanja wa King Power, ingawa wakati huu alikuwa mlishaji. Pasi yake kwa Martial nafasi ya kipindi cha pili ilikuwa nzuri, kadhalika alimtengenezea Lingard nafasi ya goli la kwanza. Nafasi zote alizotengeneza zilistahili kuwa goli.
0 comments:
Post a Comment