Wednesday, December 20, 2017

Olivier Giroud anatarajiwa kuikosa mechi ya Arsenal dhidi ya Liverpool siku ya Ijumaa baada ya kuumia misuli ya nyuma ya paja katika mechi ya ushindi wa 1-0 dhidi ya West Ham jana Usiku.

Straika huyo wa kimataifa wa Ufaransa alilazimik kutoka Uwanjani dakika 13 kabla ya mpira kuisha mechi ya kombe la Carabao.

Giroud nafasi yake ilichukuliwa na kijana Reiss Nelson na sasa anakabiliwa na kuwa nje ya dimba kwa kipindi kirefu.

Mechi ijayo ya Gunners ni dhidi ya Liverpool na Arsene Wenger anatarajia Giroud kuikosa mechi hiyo ambapo klabu ikifanya uchunguzi kujua ukubwa wa jeraha hilo.

" Inaonekana mbaya sana kwake. Nafikiri hatocheza mechi ya Ijumaa usiku." " Siku hizi unafanyiwa 'scan' saa 48 baada ya mechi. Hilo litafanyika siku ya Alhamisi na hapo ndio tutajua zaidi ni gredi gani ya jeraha hilo."

" Ukimsikiliza maumivu yanonekana ni makubwa sana" alisema wenger.

0 comments:

Post a Comment