UpSIMBA YAKIRI KUMUHITAJI ASANTE KWASI, YATUMA BARUA LIPULI
"Ni kweli tunamuhitaji Asante Kwasi kwaajili ya kuja kucheza Simba, na sasa tumepeleka barua rasmi Lipuli FC baada ya TFF kuongeza muda wa usajili.
Nawahakikishia wadau wote wa soka kwamba Kwasi akija Simba atakuwa amekuja kihalali, hawezi kuja kwa njia isiyo halali". Hiyo ni kauli ya mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zakaria Hanspoppe.
Hanspoppe pia amezungumzia wachezaji walioachwa Simba akithibitisha kumuacha mchezaji mmoja pekee ambapo amesema "Mchezaji aliyeachwa Simba ni Mwanajali peke yake, hakuna mchezaji mwingine aliyeachwa au aliyeongezwa Simba zaidi ya Kwasi". (Azamtv)
0 comments:
Post a Comment