Friday, December 29, 2017

Southampton inataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na Uingereza Daniel Sturridge, 28, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. (Telegraph)

Klabu hiyo pia inataka kutumia fedha zake ilizopata baada ya kumnunua beki wa Uholanzi Virgil van Dijk's ili kumrudisha mshambuliji wa Arsenal Theo Walcott. (Mirror)

Real Madrid wana hamu ya kumsajili beki wa kushoto wa Fulham na Uingereza Ryan Sessegnon.
Manchester United na Tottenham pia zina hamu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 (AS via Talksport)

Mabingwa wa Uhuspania Real Madrid pia wanamtaka kipa wa Chelsea Thibaut Courtois na timu hiyo ya ligi ya Uingereza iko tayari kumuuza mchezaji huyo wa Ubelgiji iwapo atakataa kandarasi mpya katika uwanja wa Stamford Bridge (Sky Sports)

Arsenal inajiandaa kumnunua winga wa Algeria na Leicester Riyad Mahrez, 26, huku mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez akitarajiwa kuondoka katika klabu hiyo (Le Buteur - in French)

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa mazungumzo ya kuandikisha kandarsi mpya ya kiungo wa kati Jack Wilshere, 25, yamepangiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Januari. (Mail)

Manchester City itataka kumsajili beki wa kati wa West Brom na Ireland kaskazini Jonny Evans, 29, ama beki wa Real Sociedad Inigo Martinez mwezi Januari. (Telegraph)

Juventus imekataa ombi la klabu ya Manchester United la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Argentina Paul Dibala kwa dau la £70m.

United imesema kuwa iko tayari kumuachilia kiungo wa kati wa Armenia Henrikh Mkhitaryan, 28, katika mpango huo.(Sun)

West Ham iko tayari kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ujerumani Andre Schurrle, 27, kwa mkopo mwezi Januari. (Guardian)

Mkufunzi wa West Ham David Moyes huenda akawasilisha ombi la kiungo wa kati wa Stoke na Wales Joe Allen. (Mirror)

Wolfsburg inataka kumsajili kwa mkataba wa kudumu mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alijiunga na klabu hiyo ya Bundesliga kwa mkopo mwezi August. (ESPN)

Stoke inataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Danny Ings, 25, kwa mkopo , lakini itakabiliwa na ushindani kutoka kwa Newcastle, West Ham na West Brom. (Independent)

0 comments:

Post a Comment