Friday, December 29, 2017

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa haogopi kumpoteza Alexis Sanchez mnamo mwezi Januari licha ya mshambuliaji huyo kuifungia Arsenal mabao mawili dhidi ya Crystal Palace.

Baada ya Andros Townsend kusawazisha bao lililofungwa na Shkrodan Mustafi katika kipindi cha kwanza , Sanchez alifunga mabao mawili.

Mshambuliaji huyo wa Chile alificha mkwaju mkali karibu na mwamba wa goli na kufanya mambo kuwa 2-1 kabla ya kuongeza bao la pili kupitia pasi nzuri iliopigwa na kiungo wa kati Jack Wilshere.

James Tomkins alifungia Palace bao la pili katika dakika za lala salama lakini mabao hayo ya Sanchez yalitosha kuipatia ushindi Arsenal ambayo sasa iko katika nafasi ya sita katika jedwali la ligi ikiwa sawa kwa pointi na Tottenham ambao wako katika nafasi ya tano na pointi moja nyuma ya Liverpool iliopo katika nafasi ya nne.

Kandarasi ya Sanchez inakamilika mwishoni mwa msimu huu na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amehusishwa na uhamisho kwa viongozi wa ligi Manchester City ambao walishindwa kumsajili katika dirisha la uhamisho lililopita.

''Siogopi, lakini hilo kitakuwa swala la baadaye kutokana na hali ya kandarasi yake'', alisema Wenger, ambaye alifikisha idadi ya mechi 810 alizosimamia katika ligi ya Uingereza sawa na aliyekuwa mufunzi wa Manchester United Sir Alex Furguson.

0 comments:

Post a Comment