Thursday, December 21, 2017

Yanga ni miongoni wa vilabu 30 bora barani Afrika kulingana na orodha iliyotolewa na shirikisho la soka barani Afrika CAF.

Yanga ikiwa timu pekee kutoka Tanzania iliyoingia kwenye orodha hiyo inashika nafasi ya 23 ikiwa imepanda kwa nafasi sita kutoka kwa mwaka uliopita.

Al Ahly ya Misri ndio inashika nafasi ya kwanza huku TP Mazembe ya DRC ikikamata nafasi ya pili.

Esperance, Etoile Du Sahel, El Hilal na Zamaleki zinakamilisha orodha ya vilabu vinavyoshika nafasi sita za juu.

Pongezi kwa wote waliofanikisha kupanda nafasi.

0 comments:

Post a Comment