Sunday, January 7, 2018

Mwandishi na Mchambuzi wa soka la Hispania kupitia kituo cha Sky Sports Guillem Balague amesema Barcelona wanatarajiwa kutumia fedha zaidi kwenye safu ya ushambuliaji.

Lakini mpango wao wa kumsajili Antoine Griezmann kutoka Atletico Madrid utasubiri hadi mwishoni mwa msimu. " Hiyo itasubiri mpaka majira ya kiangazi .

Thamani yake kwa sasa kwenye mkataba wake ni Euro Milioni 200 . Ikifika Julai Mosi itapungua hadi Euro Milioni 100 na Atletico Madrid tayari wameshakubali kwamba Griezmann atataka kuondoka."

" Ni wazi kwamba Barcelona wamejaribu kumsajili , kumekuwa na mazungumzo - chakula cha pamoja na familia ya Griezmann wakiwa na wakurugenzi wa Barcelona."

0 comments:

Post a Comment