Uamuzi wa Liverpool wa kumuuza Philipe Coutinho kwenda Barcelona hautorudisha mpango wao wa kumsajili Thomas Lemar kutoka Monaco dirisha hili la usajili la Januari, kwa mujibu wa taarifa kutoka Sky Sports.
Winga huyo wa Monaco amekuwa akihusishwa sana na kuhamia Ligi kuu ya soka ya Uingereza ambapo Arsenal nao wamehusishwa sana kumnasa Lemar mwenye umri wa miaka 22.
Kocha wa Gunners Arsene Wenger wiki iliyopita alikanusha kutaka kumsajili Lemar.
Taarifa zingine kutoka Sky Sports zinasema kwamba winga wa klabu ya Sporting Lisbon , Gelson Martins naye hayupo katika mipango ya Liverpool , taarifa hiyo imekuja baada ya Liverpool kuhusishwa na winga huyo kuja kuziba nafasi ya Coutinho.
0 comments:
Post a Comment