Thursday, January 4, 2018

Mshambuliaji nyota wa Timu ya Tanzania Taifa stars na Timu yake anayoichezea nchini Morroco Difaa al Jadida  Simon Msuva ametua nchini kwa ajili ya mapumziko na kusema atapambana hadi apate nafasi ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Winga huyo amesema amerejea nyumbani kwa ajili ya mapumziko ya wiki moja na nusu na atautumia muda huo kuwa karibu na Familia yake.

Katika hatua nyingine Msuva amesema viwango vya Tanzania katika Fifa ni sehemu ya kikwazo lakini hatakubali kushindwa.

Amesema kuwa ataendelea kupambana ili afikie ndoto yake ya kucheza Ulaya, pia ameelezea namna alivyoweza kuumia baada ya matokeo mabaya ya Timu ya Taifa katika mashindano ya CECAFA ya Nchini Kenya yaliyo malizika siku chache zilizopita.
.
"Niliumia sana kuona timu yangu ya Taifa imefanya vibaya katika mashindano ya CECAFA pale Nchini Kenya lakini  wachezaji wenzangu tusife Moyo nafasi bado tunayo ya kuleta furaha kwa Watanzania kupitia Timu yetu ya  taifa"amesema Msuva

0 comments:

Post a Comment